Om Siri ya Kifo
Hiki kitabu Siri ya Kifo ni sehemu ya kazi kubwa ambayo awali iliandikwa kwa ajili ya Kanisa linalo zungumza Kiswahili. Inachungua kwa kina dhana ya kifo, kuwa siyo mwisho wa yote. Na kama vile jambo la kushangaza kwa jinsi inavyo eleweka na wengi, kwamba kifo ni tukio ambalo kiutabibu linasababishwa na ubongo kukoma utendaji wake, lakini ndani humu tutakuonyesha kifo kuwa ni roho hai.
Tutaifanyia uchochezi itikadi ya toharani kuwa siyo ya Kikristo. Pia tutakuonyesha kifo cha mtu hakijapangwa juu yake. Wakati ukiwa unakazana na haya, utajikuta ukipokea uwezo wa kufunza wenzi wako: kifo ni nini and wapi kilitokea. Pia utapokea ujuzi wa kimaandiko kujibu kama Mbinguni, Kuzimu na Gehena (Jehanamu) kweli kupo au lah. Ndipo sasa tutakufunulia upi ni urefu wa maisha ya mtu alio pangiwa mtu hapa duniani. Ufupisho huu ni finyu sana, na umeacha mambo mengi tatanishi na tete juu ya suala zima la kifo.
Vis mer